BWANA AKUFUNDISHE KUOMBA

“Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.” Luka 11:1

Wanafunzi wa Yesu waliona namna ambavyo wanafunzi wa Yohana mbatizaji wakiomba,kisha wakapenda namna walivyokuwa wakiomba. Lakini baadae waligundua kwamba kuna utofauti kubwa kati yao na wanafunzi wa Yohana mbatizaji kwenye eneo la maombi.

Bila shaka walipojipima waliona wanafunzi wa Yohana mbatizaji wana kitu fulani cha ziada katika uombaji wao,kitu ambacho wao hawakuwa nacho. Ndiposa wakamwomba Bwana awafundishe kusali kama wanafunzi wa Yohana walivyofundishwa.

Ombi lao lilikuwa ni zuri sana,kwa maana kwa ombi hili walionesha kuwa walikuwa ni watu wenye kiu ya kufundishwa kuomba ipasavyo.  Hivi ndivyo inavyokupasa wewe kumwomba Roho akufundishe kuomba

Wanafunzi wa Yohana mbatizaji walifundishwa “namna ya kuomba” kisha wanafunzi hao wakayafanyia kazi mafundisho. Walipoomba walionekana wazi kwamba ni wanafunzi wa Yohana mbatizaji,wanaomba kama walivyofundishwa. Hata kama wanafunzi hao wang’elichangamana na wanafunzi au watu wengine bado kulikuwa na alama / identinty iliyowatambulisha kwa habari ya uombaji wao.

Kumbuka;

Yohana mbatizaji alikuwa mwombaji mzuri na mwalimu wa maombi mwenye kuweza kusababisha muambukizo / impartation katika maombi. Alikuwa ana tabia ya kujificha / si ya kujitangaza. Tabia ya mwombaji ni tabia ya maficho kwa maana mwombaji mzuri kamwe hajitangazi,bali watu watayaona matendo yake tu.

  • Maombi yanafundishika

Kitu ambacho watu wengi hatuelewi ni kuhusu shule / darasa la “ maombi’‘ . Uombaji mzuri hauji automatically bila kupitishwa kwenye shule ya maombi. Wanafunzi wa Yohana mbatizaji walipitishwa kwenye shule ya maombi,hatimaye wakawa waombaji wazuri kiasi cha kutamaniwa na waombaji wengine. Shida kubwa tuliyonayo leo,weatu hawapendi shule hasa shule ya kujisimamia wao wenyewe kwenye maombi bali wengi hupenda kuombewa tu.

  • Roho mtakatifu mwalimu wa maombi

Wakati wa Yohana mbatizaji wanafunzi wake aliwapitisha katika shule ya maombi,lakini sasa shule ya maombi hufundishwa na Roho mtakatifu mwenyewe. Hivyo Roho mtakatifu ndiye mwalimu mzuri afundishaye – Warumi 8:26. Hivi unajua kuna wakati fulani wa maisha hujui wala huelewi uombaje,kwa maana maneno yanakukosa! Hapo….

INAENDELEA KUCHAPWA,… ENDELEA KUTEMBELEA HAPA.

2 thoughts on “BWANA AKUFUNDISHE KUOMBA

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.