MAISHA YA ADAMU – 1

“ Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.’’ Mwanzo 2:7

  • Kuumbwa kwake

Binadamu wa kwanza ulimwenguni,Adamu na mkewe Hawa. Wote wawili waliumbwa kwa wakati na muda unaofanana katika ulimwengu wa roho ( Mwanzo 1:27)

Kwa mujibu wa biblia,alipoumbwa mwanaume ndipo mwanamke naye akaumbwa. Lakini katika ulimwengu wa mwili tunaona Adamu alitolewa kwanza ,kisha Hawa alifuata.

Adamu alikuja ulimwenguni akiwa mtu mzima ( Hawa naye ni vivyo hivyo),mwanamume kamili,yaani kila kitu kinafanya kazi kama mwanaume mwenye akili na mwenye kuweza kuchukua majukumu yake papo hapo alipoletwa ulimwenguni,

Hii ni tofauti na ujio wa wanadamu wote,kwa maana sisi wanadamu ni lazima tuzaliwe katika hali ya uchanga , kisha ndipo taratibu tunaanza kuku ahata kufikia utu uzima.

Lakini pia Adamu hakuzaliwa na mwanamke yoyote bali aliumbwa moja kwa moja,
sisi sote tukija duniani ni lazima tuzaliwe na mwanamke.

Adamu alipoumbwa tu,alikuwa na uwezo wa mara moja wa kumtambua Mungu aliyemuumba na aliweza kumsikia

Kwa sehemu ndogo sana Mungu amewawezesha watoto wachanga uwezo wa kujua kwa haraka sauti za mama zao au kuwatambua. Ndio maana mtoto aliyezaliwa na hatimaye,

akaishi na mama yake japo kwa muda fulani anaweza akajua sauti ya mama yake,hata kumtambua,ikiwa kichanga hicho kitabebwa na mtu mwingine ambaye si mama mzazi basi ni dhahiri kuashilia amebebwa na mtu ambaye si mama yake mzazi.

Adamu hakuitaji afundishwe kumjua Mungu,wala kumsikia kama leo tunavyopata shida ya kujifunza namna ya kumjua na kumsikia Mungu.
Adamu alipozaliwa kwa kuumbwa,kila kitu kilikuwa tayari kinamsubiri yeye kama mtawala.

Ni sawa na kusema ulimwengu na unono wake ulikuwa tayari unamsubiri mtawala.
Adamu alipoletwa duniani katika dakika ile ile,“hakulia’’ kama Watoto wachanga leo wakizaliwa ni lazima walie.

Na endapo kama mtoto aliyezaliwa,halii basi wakunga watatafuta njia mbadala ya kumfanya mtoto / kichanga kilie ndipo mambo mengine yaendelee
maana kisipolia ni hatari anaweza akawa bubu au kukosa akili timamu,n.k.

Lakini Adamu hakulia na bado akili zake zilikuwa nyingi kiasi kwamba hazikuweza kupimika
Dunia inawaka moto kwa maovu,

kichanga kikiacha enzi yake kutoka huko tumboni kwenye ulimwengu usiokuwa na uharibifu,siku hiyo kikija duniani kwenye ulimwengu wa uovu na dhambi hapo kitoto lazima kipige kelele na kulia

  • Ndoa ya Adamu

Adamu aliletewa “mke’’ anayefanana naye kwa maana haikuwa vyema yeye kuwa peke yake ( Mwanzo 2:18). Mkewe Hawa alitoka kwa Bwana moja kwa moja kwa sababu hiyo Adamu hakutumia nguvu binafsi kumtafuta mkewe bali nguvu iliyotumika ilikuwa ni nguvu ya Mungu.

Tunapata somo hapo kumbe mke / mume anapaswa aletwe na Mungu mwenyewe. Akili na nguvu zako binafsi hazihitajiki katika kutafuta mwenza wako!

Ingawa biblia haisemi Hawa mwanamke alifinyangwa baada ya muda gani tangu Adamu alipofinyangwa.

Lakini siku ile Hawa mwanamke alipouumbwa kwa jinsi ya mwili,siku hiyo hiyo ndoa ilifanyika kati ya Adamu na Hawa, yaani Adamu alioa siku hiyo hiyo,hatimaye wakawa mume na mke.

Mungu mwenyewe aliwafungisha,Kumbe ndoa halisi ni lazima “Mungu mwenyewe ausike,ndiye awafunge mtu mume na mtu mke na kuwa mwili mmoja’’ – Kwa sababu ndoa ni wazo la Mungu mwenyewe.

Ndoa ya Adamu na Hawa ndio ndoa ya kwanza kabisa ulimwenguni mwote. Ndoa hii ni ya mume mmoja na mke mmoja,Kumbe tangia mwanzo ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja ( Marko 10:6)

ITAENDELEA

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.

Kwa msaada zaidi unipigie simu +255 781 001 002

What’s app number +255 746 446 446

Na Mch. Gasper Madumla

UBARIKIWE.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.