KUPANDA MBEGU NA BWANA – 4

3. Ombea sadaka za mbegu zako vizuri 

Sadaka ya mbegu inahitaji maombi ya kina.  Pamoja na mchungaji aweza kukuongoza wakati wa ibada ya kupanda mbegu, lakini mpandaji / mtoaji anapaswa awe na maombi yake binafsi kwa sababu ni yeye ndiye hasa mtoaji

4. Hakikisha unampa nafasi ya kutosha Roho Mtakatifu

Yeye Roho mtakatifu ndiye atakayekuongoza katika kila kitu, hivyo ni vyema ukampa nafasi akuongoze.  Ukimpa nafasi Roho utashangaa kwa maana atakusemesha ndani juu ya sadaka ya mbegu na kwa namna gani unapaswa kutoa

5. Andika maombi yako bila majina yako

Ikiwa sadaka ya mbegu unaitoa kanisani mwako, basi ni vyema kuandika maombi yako machache yale ambayo ni muhimu sana.  Kisha baada ya kuandika, tumbukiza ndani ya bahasha yenye sadaka yako

6. Upande mbegu kwa watoto wako

Kila mtoto unamwekea bahasha yake ya sadaka ya mbegu na kumtolea.  Kwa kuwa kila mtoto anakusudi lake tofauti basi hakikisha unamtolea kila mtoto sadaka yake. 

Mambo muhimu ya kufahamu

1. Apandaye hapa atavuna hapa  ( 2 Wakorintho 9:6)

1.Ukweli ni kwamba utavuna utakachokipanda,  lakini ikiwa utapanda kwa uchache utavuna pia kwa uchache.  Hata tunapotoa sadaka zetu za mbegu, kama tutatoa kwa uchache na vilivyo vinyonge tutavuna uharibifu.

Kumbuka;  Ukipandacho ndicho utavuna. Angalia mifano hii;

  • Rahabu aliyekuwa kahaba alipanda ““” ukarimu” akavuna ukarimu – Yoshua 2 -4 yote
  • Kornelio alipanda sadaka za ” msaada” kwa watu wengi,akavuna ” msaada wa wokovu ” – Matendo 10:2,34-48
  • Akida alipanda sadaka ya ujenzi wa Sinagogi, watu wakamlingana Mungu, alipouguliwa na mtumwa wake,alivuna uzima kwa kuponywa mtumwa wake -Luka 7:2-10

Hivyo, chochote utakachopanda ni lazima uvune.  Hii inatuambia kwamba sadaka yoyote unayomtolea Bwana “haipotei ” Bali itakuletea mavuno kwa wakati wa Bwana.

2. Utavuna wakati usiotegemea wala kujua – Marko 4:26-27

Kawaida ya Mungu ni kukushangaza,Hivyo sadaka ya mbegu unayomtolea leo, utakuja kuvuna matunda yake bila kujua, bila kutegemea.

Hivi unajua matunda yajapo kwenye mti hayapigi kelele kwamba “tunakuja”Bali yatakuja pasipo mkulima kujua,kwani Kuna siku atakuja kuona kwamba mti umeanza kutoa matunda.  Kwa sababu kazi ya kutoa matunda / kazi ya kukuza ni ya Bwana si ya mkulima – 1 Wakorintho 3:6

3. Sadaka ya mbegu lazima iambatane na nia ya mtoaji – Ayubu 1:5

Moja wapo ya tofauti kati ya sadaka za kawaida na sadaka ya mbegu ni kwamba sadaka za kawaida hazibebi nia ya mtoaji lakini sadaka ya mbegu itamdai mtoaji awe na sababu maalumu ya sadaka yake.  Yaani unatoa sadaka ya mbegu kwa sababu gani?  Nini kinakusukuma hata kutoa sadaka ya mbegu?

Angalia mfano;

Ayubu aliwatolea sadaka wanae. Biblia inatuambia nia / sababu ya Ayubu kuwatolea sadaka wanae ilikuwa ni “kuwatakasa ” . Hivyo sadaka yake ilikuwa sadaka kwa ajili ya “toba”

Vivyo hivyo na kwako, unapoandaa sadaka ya mbegu basi hakikisha unakuwa na nia binafsi.

Faida ya kupanda mbegu na Bwana

  • Kugeuza uteka / kubadili mfumo wa maisha – 1 Wafalme 17:10-16
  • Ukumbusho mbele za Bwana – Matendo 10:4
  • Kuvuna zaidi ya mara moja – Mathayo 13:8
  • Mibaraka zaidi “kuzidishwa ” -2 Wakorintho 9:10, I saya 30:23

Mwisho.

Kwa msaada zaidi, ushauri na maombezi +255 781 001 002

What’s app +255 746 446 446

Mch. Gasper Madumla

UBARIKIWE 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.