TABIA / SIFA ZA MUNGU.

 

• Mungu ni nani ( who is the God?)

Huwezi kujibu swali hili ikiwa hufahamu tabia za Mungu. Ni swali gumu na zito. Kwa sababu Mungu ni zaidi ya unachojua sasa,hata kama utamweleza Mungu ni nani lakini nataka nikuambie huwezi ukamweleza Mungu na kummaliza. Na ndio maana sote tueleza Mungu ni nani kwa kujaribu na kujitahidi kwa kulingana na ufahamu tulionao wa kibinadamu tukiongozwa na neno lake.

Neno moja nataka ufahamu leo kwamba Mungu ni mkubwa sana,mkuu sana kiasi kwamba hawezi kulinganishwa / kufananishwa na chochote kile kwa sababu kile utakachokifananisha nacho kimeubwa na yeye.

• Mungu hawezi kupigana na shetani.

Watu husema Mungu anapigana na shetani kwa sababu hawamjui Mungu wanayemzungumzia ni Mungu wa namna gani. Ukweli ni kwamba shetani ni katoto kadogo ambacho hakana uwezo wa kupambana na Mungu kwa sababu kwanza shetani kaumbwa na Mungu huyo huyo. Sasa jiulize ; Mungu anaweza akapambana na yeyote aliyemwuumba? Hivyo ukiona mapambano yoyote ujue shetani anapambana na watoto wa Mungu tu na sio Mungu mwenyewe. Unaelewa lakini? Hadhi ya Mungu ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi akashindani na yoyote yule!

Tabia za Mungu zipo za aina mbili;

  1. Tabia / sifa za Mungu binafsi ( incommunicable attributes)
  2. Tabia / sifa shirikishi. ( communicable attributes)

01.Tabia binafsi ( Incommunicable attributes)

Hizi ni zile tabia ambazo Mungu hamshirikishi yoyote bali ni za kwake tu. Au ni zile tabia / sifa za Mungu ambazo huwezi kuzikuta kwa mwanadamu bali ni Mungu tu ndio mwenazo na kupitia tabia hizi ndio maana Yeye akaitwa Mungu. Ni hizi hapa;

• Umilele ( Eternity ) – Zab. 90:2,Ufunuo 22:13 na Mwanzo 1:1

Mungu hana mwanzo wala mwisho. Yeye alikuwepo,yupo na ataendelea kuwepo,hukaa milele. Hii ni tabia ambayo ni ya kimungu tu. Hata mwanadamu hana tabia / sifa hii kwa maana mwanadamu alizaliwa naye atakufa. Ukweli ni kwamba kila kitu kimekuwa na mwanzo na kimekuwa na mwisho,isipokuwa Mungu tu,asiyekuwa na mwanzo wala mwisho. Yeye yupo tangu mwanzo na atakuwepo milele.

• Hana mipaka / Hasiyezuiliwa na nafasi ( Omnipresence ) – Zab.139:7-10,Yeremia 23:23-24

Mungu hazuiliwi na mipaka bali kila mahali yupo hapa hapa yupo pia kule. Ebu fikiria; leo Dar Tanzania tunaomba,papo hapo Marekani New york sasa hivi na wao wanaomba,muda huu huu huko China na wenyewe wanaomba Mungu huyo huyo mmoja. Yupo kila sehemu. Mwanadamu hawezi kuwa na tabia au sifa kama hii.

• Asiyebadilika ( Unchangeableness ) -Malaki 3:6. Zab.33:11.

Moja wapo ya tabia ya kila mwanadamu ni kubadilika badilika. Yaani kuwa kigeu geu. Utakuta leo unasema hili,kesho umebadili na kusema jingine na mbaya zaidi unakataa kabisa kama ulisema hata kama wamekurekodi lakini bado unasema “ mimi sikusema hivyo,labda hamkunielewa “

• Asiyechoka ( Isaya 40:28)

Hii ni sifa nyingine ya kipekee aliyonayo Mungu wetu tunayemwabudu. Mwanadamu huchoka,tena uzimia lakini Yeye Bwana Mungu hachokii wala hazimii,wala akili zake hazichunguziki.

• Mwenye uhuru katika utendaji kazi ( Independence ) – Matendo 17:24-25 Yeye haitaji msaada wa namna yoyote, bali yupo na uhuru wa kutenda chochote atakacho.

02. Tabia / sifa shirikishi ( Communicable attributes)

Sifa au tabia shirikishi ni zile ambazo unaweza kuziona kwa mwanadamu pia. Kama vile;

• roho / Mungu ni Roho. ( Spirit ) Yoh. 4:24.

Sifa hii tunaiona kwa mwanadamu pia kwa kuwa wewe ni roho mwenye nafsi unayeishi kwenye mwili. Sifa hii Bwana ametushirikisha sisi pia.

• Pendo ( Love) – 1 Yoh. 4:8.

Hivi unajua,Yeye mwenyewe ni Pendo. ? Ndio ,Mungu ni pendo na ni sifa yake pia. Katika sifa hii ametushirikisha / sifa hii inapatikana kwetu.

• Utakatifu ( Holiness ) 1 Petro 1:15-17

Yeye Mungu ni mtakatifu sana,na utakatifu ni sifa yake. Katika hili,wewe pia unaweza ukawa mtakatifu kama Mungu atakaa hapo hapo. Suala la utakatifu linawezekana kwako ndio maana unaambiwa uwe mtakatifu.

• Uaminifu na utu wema ( Faithfulness & Kindness) Hesabu 23:19

Nimekuandikia sifa chache zitakazo kukusaidia katika ufahamu wako. Zipo nyingi sana sifa za Mungu, kiasi cha kushindwa kuziandika moja hata kuzimaliza. Lakini katika hizi nilizokuandikia,ebu zipitie tena kiundani kisha zishike ili zikusaibia.

Ikiwa fundisho hili limekubariki na umejifunza kitu,nifahamisha tumtukuze Mungu pamoja

Kwa maombi, maombezi na ushauri ; ( + 255 ) 0781 001 002

WhatsApp ni +255 746 446 446

Mch. Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

14 thoughts on “TABIA / SIFA ZA MUNGU.

    1. Shalom pastor, pole na hingera kwa kazi ya Mungu. Binafsi nahitaji kujua hasa tofauti ya TABIA na SIFA za MUNGU. Naomba kujifunza.

      Like

  1. Shalom pastor, pole na hingera kwa kazi ya Mungu. Binafsi nahitaji kujua hasa tofauti ya TABIA na SIFA za MUNGU. Naomba kujifunza.

    Like

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.