KUPANDA MBEGU NA BWANA – 3

  • Kanuni ya kupanda mbegu na kuvuna

Kumbuka,

Huwezi kuvuna ikiwa kama hujapanda. Yeye avunae ni yule aliyepanda. Lakini pia apandae haba atavuna hapa ( 2 Wakorintho 9:6 ). Hii ina maana huwezi kuvuna zaidi ya kile ulichopanda,mkulima anayehitaji kuvuna kwa ukubwa hana budi kupanda kwa ukubwa. Pia ukitaka kuvuna vizuri huna budi kuzingatia kanuni bora za upandaji, zifuatazo ni baadhi tu ya kanuni za msingi za kupanda mbegu na Bwana;

1. Andaa mbegu

bora Kuna mbegu kama mbegu na kuna “mbegu bora” Upatikanaji wa mbegu ni rahisi lakini upatikanaji wa “mbegu bora” si rahisi kwa maana mbegu bora inatafutwa. Uvunaji wenye tija utegemea ubora wa mbegu,hivyo mbegu ndio kila kitu katika suala la kupanda na kuvuna.

Ndio maana mkulima wa kawaida akitaka kuvuna mazao mengi atahakikisha anatumia muda mrefu katika kuandaa mbegu bora,atajifunza kupitia tafiti mbali mbali zilizofanywa na kutolewa na vituo vya utafiti wa mazao ya kilimo ili kusudi apate kujua mbegu bora ni mbegu ya namna gani na kwa namna gani anaweza kuipata. Suala hilo la utafiti na kujifunza katika tafiti mbalimbali ni suala linalohitaji muda mrefu,lakini mkulima ataendelea kutafuta mbegu bora

Hivyo mkulima yupo makini kutafuta mbegu bora kwa sababu hataki kupata hasara. Kama alivyo mkulima huyo,ndivyo inavyopaswa wewe ambaye ni mkulima wa kiroho unapaswa kuwa makini sana na mbegu unayotaka kupanda na Bwana.

Sadaka yako ya mbegu ni lazima iwe ni sadaka yenye thamani machoni pa Bwana Mungu,wala isiwe ni sadaka yoyote tu!Ni vyema kusisitiza hili kwa sababu watu wengi wanapotoa sadaka hawana maandalizi ya sadaka.

  • Sadaka nzuri inahitaji maandalizi

Sadaka haiandaliwi wakati wa kutoa bali inaandaliwa wiki moja kabla, wakati wa kutoa,unatoa kile kilichoandaliwa. Leo wengi wanaposikia mchungaji anahitisha sadaka basi huo ndio wakati wanautumia kupekua pekua mfukoni,

au kwenye pochi kisha kile kitakachopatikana ndicho kinatolewa tena ikiwa kama mtoaji aliishika noti ya tshs 10,000 au noti ya pesa kubwa,mara nyingi ni lazima ataihurudisha kisha na kutafuta pesa ndogo,akiipata ataitoa kama sadaka!!!!

2. Andaa shamba vizuri

Shamba lolote linalohitaji kupandwa mbegu ni lazima liandaliwe ipasavyo. Moja ya maandalizi makubwa ya shamba ni kulima,kungo’a magugu, na kupalilia. Hata hivyo kuna maandalizi mengi yanayofanyika kabla ya kupanda.

Baada ya kuvuna mkupuo wa kwanza basi shamba liandaliwe kupokea mbegu mpya,kama halitaandaliwa mbegu inaweza ikawa ni mbegu bora,lakini iakafa mapema,magugu ni adui wa ukuaji! Tunapokusudia kupeleka sadaka zetu za mbegu mbele za Bwana hatuna budi kuandaa madhabahu kama shamba letu la kupandia

Kama ilivyo katika shamba la kawaida,mkulima atalima,atango’a,atapalilia kisha ndipo apande ndivyo ilivyo tunavyopeleka mbegu zetu kwa Bwana,madhabahu ni lazima andaliwe kwa maombi. “maombi ya toba” ni maombi ya kuisafisha madhabahu kama mtu asafishavyo shamba ili kuruhusu mbegu kupandwa.

Maombi ya toba yanaifanya ardhi kuwa safi,lakini pia “maombi ya kungoa na kubomoa” yanangoa mapando yote kwenye madhabahu ili na kuifanya madhabahu kuwa tayari kupokea mbegu. Watu wengi wanajua kwamba madhabahu inaandaliwa na wachungaji peke yao,

hawajui na wao wanaopeleka sadaka zao wanahitajika kuiandaa madhabahu. Maombi ya wachungaji yanahitajika sana kwa sababu ndio waliokabidhiwa madhabahu lakini pia wewe ambaye ni mkulima wa kiroho / mpanzi unahitajika.

Hivyo maandalizi ya shamba ni kanuni muhimu sana kwa sababu mbegu bora huitaji shamba lililoandaliwa vizuri. Lakini pia kama huna shamba la kupandia mbegu zako,basi ni vyema utafute shamba kwanza ili kuepuka kupanda kwenye shamba lolote! Ndivyo ilivyo hata utoaji wa sadaka ya mbegu,kuna watu hawana madhabahu ya kupeleka sadaka zao.

Mioyoni mwao kuna kataa ikiwa wanataka kupanda/ kutoa sadaka zao mahai fulani,basi ni vyema kwanza moyo ukubali shamba / madhabahu gani ya kupeleka sadaka zako. Ikiwa hali iko vile vile inakataa , basi ujue unahitaji msaada wa kiroho haraka.

Waweza kunipigia simu leo ili tutafute kujua kwa nini moyoni kuna goma kupeleka sadaka zako kwenye madhabahu fulani

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.

Kwa msaada zaidi unipigie simu +255 781 001 002

What’s app number +255 746 446 446

Na Mch. Gasper Madumla

UBARIKIWE.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.