NAMNA YA KUITAWALA HASIRA

Hasira ni hisia kali ndani ya mtu zinazosababishwa hasa na kuumizwa ambapo hisia hizi kama hazijathibitiwa ndani,basi zinajitokeza nje na kumpelekea mtu kuchukua hatua fulani labda kulia kwa uchungu,kungata meno,au kufanya jambo fulani. Kawaida mfumo wa viungo vyetu hushirikiana kila kimoja. Hivyo hisia kali zinapotoka nje,basi kila kiungo kinashirikiana na kingine kuelezea nini kinachotoka nje.… Read More NAMNA YA KUITAWALA HASIRA

MADHARA YA KUAMBATANA NA WATU WASIO SAHIHI

Ukweli ni kwamba watu wanaokuzunguka kila siku,wana sehemu kubwa sana katika maisha yako. Hii ni sawa na kusema kwamba,watu wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana katika hatma yako, Kwa maana kupitia wao wanaweza kukusaidia kupiga hatua, ambalo ni jambo jema. Lakini kupitia wao unaweza ukacheleweshwa,ukakwama katika mambo mengi. Jifunze machache kupitia picha ya hapo juu,kabla ya… Read More MADHARA YA KUAMBATANA NA WATU WASIO SAHIHI

MALAIKA WA BWANA ATAKUTANGULIA MBELE YAKO

“Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.” Kutoka 23:20 Andiko hili,linatueleza kuhusu upendo wa Mungu kwa watu wake wamchao kwa kumtuma malaika wake mwenye kwenda mbele yao,ili awalinde. Ukweli ni kwamba Bwana hataki mtu wake hata mmoja apotee kwa namna yoyote ile. Moja kati ya jambo… Read More MALAIKA WA BWANA ATAKUTANGULIA MBELE YAKO

TOSHEKA NA MSHAHARA WAKO.

  Wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa,Neno la Mungu lilimfikia Yohana mwana wa Zakaria,akiwa jangwani. Naye Yohana tangu wakati huo,akaanza kuhubiri juu ya ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Yohana alifahamika kwa kazi yake,naye huitwa Yohana mbatizaji,mtu shupavu,aliyejazwa Roho mtakatifu tangu tumboni mwa mamaye,mtengeneza njia ya Bwana. Yohana, aliulizwa maswali mengi na… Read More TOSHEKA NA MSHAHARA WAKO.

MUNGU KAMILI NA MWANADAMU KIMILI ~ 2 ( tamati)

  …kitendo cha kuitwa “mwana wa Mungu” kinaonesha hali yake ya uungu alionao. Huku uswahili kwetu ( Tz) tunamsemo usemao “mtoto wa nyoka ni nyoka” msemo huu ni wa wahenga ambao walikuwa wakijaribu kusema kwamba mtoto wa nyoka ana tabia sawa na nyoka mkubwa,wanafanana hata tembea yao. Ni sawa na kusema ukimwona mtoto wa nyoka,umemwona… Read More MUNGU KAMILI NA MWANADAMU KIMILI ~ 2 ( tamati)

CHUKI.

Neno hili“chuki”ni neno dogo sana lakini lina matokeo makubwa sana. Sikudhani kama “chuki” limebeba mambo mengi kiasi hiki. Hivyo ni vyema tutafakari kuhusu “chuki ” ,ili tupone! Awali ya yote chuki ni kinyume cha upendo. Na ndio maana ukisikia mtu akisema “fulani anakuchukia…” basi maana yake “fulani hakupendi..”. Hata hivyo,tunaweza kuitasfiri tena chuki kama hisia… Read More CHUKI.

HUKUJA NA KITU DUNIANI,TENA HUWEZI KUTOKA NA KITU.

  Kuna siku moja niliona tukio moja kwenye tarevisheni / TV likanishangaza kidogo,lilikuwa ni tukio la mazishi ya mtu mmoja mwenye pesa nchini Nigeria. Mtu huyo katika mazishi yake,watu wa jamii yake wakaamua kumzika na baadhi ya mali zake mfano gari lake. Mimi Sikuelewa!!! Ilikuwa maigizo au ni kweli? Anyway! Wanajua wao. Lakini jambo hili… Read More HUKUJA NA KITU DUNIANI,TENA HUWEZI KUTOKA NA KITU.

KIBURI.

  Kiburi cha uzima. Fikiria mtu ambaye aombi kabisa kwa sababu si mgonjwa. Haendi kanisani kwa kuwa haoni haja ya kwenda kwa sababu ataboreka hivyo ni afadhali atume watoto waende badala yake. Au anaona ni afadhali atume sadaka zake kwenye simu kwa mchungaji lakini yeye hubakia nyumbani maana anaona shida kuchangamana na watu wengine. Fikiria… Read More KIBURI.