KUPANDA MBEGU NA BWANA – 4

3. Ombea sadaka za mbegu zako vizuri  Sadaka ya mbegu inahitaji maombi ya kina.  Pamoja na mchungaji aweza kukuongoza wakati wa ibada ya kupanda mbegu, lakini mpandaji / mtoaji anapaswa awe na maombi yake binafsi kwa sababu ni yeye ndiye hasa mtoaji 4. Hakikisha unampa nafasi ya kutosha Roho Mtakatifu Yeye Roho mtakatifu ndiye atakayekuongoza… Read More KUPANDA MBEGU NA BWANA – 4

PASAKA

_By Apostle Peter Mansy_ _☎️0769144366_ 0746 446 446 ( Pastor G. Madumla For more information ) _✍🏾 *Pasaka* katika lugha ya Kiebrania ni (*Pesach*) Kwa kilatini ni *”Pascha”* na kwa kigiriki pia ni *”Pasch”* na kwa Kingereza ni *PASS OVER* yaani *KUPITA JUU YA.*_ 🔵Mwanzo wa *Pasaka* Ulikuwa wakati wa mtumishi wa Mungu *MUSA* _📖Kutoka12:14_21_… Read More PASAKA

KUGEUZWA NA KUWA KAMA WATOTO WADOGO ILI KUURITHI UFALME WA MBINGUNI

“ akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.” Mathayo 18:3 Watoto wadogo wamebeba tabia halisi ambazo mtu mzima wa imani / aliyeokoka anapaswa awe nazo. Kama mtu wa imani katika Kristo akizikosa tabia hizo,basi ni dhahiri mtu huyo bado hajamjua Mungu na wokovu wake ni bure. Tabia nyingi… Read More KUGEUZWA NA KUWA KAMA WATOTO WADOGO ILI KUURITHI UFALME WA MBINGUNI

AINA TATU YA WATU UNAOWAHITAJI KWENYE HATMA YAKO – 3

“na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.” Matendo 18:3 Anayekupa michongo ya kazi au huduma Paulo alipomwona Akila akagundua kazi zao zinafanana,hivyo wakakaa pamoja katika ufundi wa kushona mahema.  Akila alimwihitaji Paulo,naye Paulo alimwihitaji Akila kwa sababu Akila alikuwa na connection… Read More AINA TATU YA WATU UNAOWAHITAJI KWENYE HATMA YAKO – 3

NIPE NAFASI YA KUWA SAUTI YAKO,NAKUPENDA

Na Mwl. Syaga James Stori ya kijana na binti walioshibana. Baada ya miaka michache, kijana huyo alihitimu kozi fupi na kuamua kuendeleza masomo yake nje ya nchi. Kabla ya kuondoka, alimwambia binti huyo: “Sina maneno mengi. Lakini, ninachojua ni kwamba, ninakupenda. Ukinikubalia, nitakutunza na kukupenda kwa Maisha yangu yote.”, Binti huyo alikubali na familia yake… Read More NIPE NAFASI YA KUWA SAUTI YAKO,NAKUPENDA

AINA TATU YA WATU UNAOWAHITAJI KWENYE HATMA YAKO – 2

Mwombezi na mtia moyo Kawaida ya watu wengi tunaokutana nao katika maisha ya kila siku ni aina ya watu wakatisha tamaa na wavunja mioyo yetu. Neno “huwezi’’ tumeambiwa mara nyingi tangu utotoni na sasa tumejikuta hatuwezi kweli lakini sio kwamba hatuwezi,bali wakatisha tamaa wameumba kushindwa na hatimaye tumejikuta tukitembea katika roho ya kushindwa Wengine wengi… Read More AINA TATU YA WATU UNAOWAHITAJI KWENYE HATMA YAKO – 2

AINA TATU YA WATU UNAOWAHITAJI KWENYE HATMA YAKO – 1

Mwinjilisti Simon Mabula wa kanisa la Beroya Church-Dar,Tanzania aliwahi kutufundisha kanisani siku moja Jumapili ya tarehe 4,Feb,2024 . Kuhusu watu tunaowahitaji katika maisha yetu ya kila siku tunapoelekea kwenye hatma zetu. Nami naona vyema nikuandikie ili nawe ujifunze  Watu wanaotuzunguka wana mchango mkubwa kutuwezesha au kutukwamisha Inawezekana hivyo ulivyo sasa ni kwa sababu ya aina… Read More AINA TATU YA WATU UNAOWAHITAJI KWENYE HATMA YAKO – 1

TOFAUTI KATI YA NDOA KAMA AGANO NA NDOA KAMA MKATABA

“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” Mwanzo 2:18 Haikupendeza mtu mume awe peke yake,kwa maana kuna mambo asingeyaweza. Hivyo umuhimu wa mtu mke ulionekana tangu hapo mwanzo. Hii ni sawa na kusema kila mmoja anamwitaji mwenzake ili kukamilisha uhusiano mzuri wa kifamilia kwa sababu chanzo cha… Read More TOFAUTI KATI YA NDOA KAMA AGANO NA NDOA KAMA MKATABA

SALAMA YAKO NI KUMTOSA YONA BAHARINI

“Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata.” Yona 1:11-12 Wakati wafanyabiashara wakiangaika kushusha shehena za mizigo kwa kuzitupa baharini hali wakijua ni hasara kwao lakini hawakuwa na namna kwa… Read More SALAMA YAKO NI KUMTOSA YONA BAHARINI

MATUMAINI NA UKOMBOZI

“Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma.Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo;Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche.” Ayubu 14:7-9 Mti uliokatwa bado haujafa ijapokuwa umekatwa,kwa maana una matumaini ya kuchipuka tena. Tena machipukizi yake hayatazuiliwa au hayatakuwa na… Read More MATUMAINI NA UKOMBOZI

FAIDA YA MAOMBI YA KUFUNGA

“Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] ”… Read More FAIDA YA MAOMBI YA KUFUNGA

BWANA AKUFUNDISHE KUOMBA

“Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.” Luka 11:1 Wanafunzi wa Yesu waliona namna ambavyo wanafunzi wa Yohana mbatizaji wakiomba,kisha wakapenda namna walivyokuwa wakiomba. Lakini baadae waligundua kwamba kuna utofauti kubwa kati yao na wanafunzi wa Yohana mbatizaji kwenye eneo la… Read More BWANA AKUFUNDISHE KUOMBA

MWOKOZI AMEZALIWA

“maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.” Luka 2:11 Kuzaliwa kwake mwokozi,masihi wa Bwana,kulikuwa kunashangaza ulimwengu,pia ilikuwa ni ajabu sana. Lakini uzuri ni kwamba kuzaliwa kwake ni kutimia kwa unabii wa kwanza wa ukombozi wa mwanadamu – Mwanzo 3:15. Kuzaliwa kwake kulitoa taarifa kwamba kuna “mwanaume” amezaliwa atakaye… Read More MWOKOZI AMEZALIWA

NGUVU YA USHUHUDIAJI

Mchungaji mmoja aliwahi kusema “ mchungaji hazai kondoo,kondoo huzaa kondoo” Lakini pia mchungaji huyo aliendelea akishuhudia namna alivyookoka,akasema“nilihubiriwa injili na kijana mdogo aliyekuja nyumbani kwangu,hatimaye  nikaokoka” Maneno haya ya mchungaji yanaonesha wazi kwamba kuna watu wengi ambao wanahitaji kufuatwa,washuhudiwe ndipo waokoke.  Hivi unajua? Watu hao wasiposhuhudiwa injili ya Bwana,kisha wakifa katika uovu wao basi Mungu… Read More NGUVU YA USHUHUDIAJI

MAOMBI YA MNYORORO – 3

Kipaumbele /ajenda ya maombi Tunafahamu kwamba maombi mazuri ni yale ambayo yanayoongozwa na vipaumbele. Vipaumbele kwenye maombi huitwa “prayer points / vipengele vya maombi’‘. Vipaumbele /prayer points za maombi ya mnyororo vinatofautiana sana na vipaumbele vya maombi.  Kwa sababu kipaumbele cha maombi ya mnyororo cha kwanza ni kushughulikia ajenda moja tu mpaka iishe ndipo ije… Read More MAOMBI YA MNYORORO – 3