UJASIRI

Ujasiri / courage” Ni uwezo wa kufanya vitu ambavyo mtu mwingine anaviogopa. Au ni hali/ kiwango cha kuwa na uthubutu kisha kutenda bila hofu. Ni uwezo wa kuwa chanya / positive na kuona kwamba unaweza kufanya kitu ambacho wengine wamesema hawawezi. Ujasiri ni kufanya kiume (1Wakorintho 16:13).

Ujasiri ni moyo kamili wa Mungu,(Yeye ndiye chanzo cha ujasiri). Lakini pia,Ujasiri ni siri ya ushindi. Biblia ni kitabu kinachoeleza “ujasiri na majasiri wa imani” tangu mwanzo wa kitabu hadi mwisho wa kitabu,watu kama akina Gideoni,Yoshua,Petro,Yohana,Paulo n.k. Kinyume cha ujasiri ni hofu na mashaka!!!

  • Ujasiri unatokea wapi?

Ujasiri umetokana na Mungu mwenyewe. Mungu hakukupa roho ya woga,bali alikupa roho ya nguvu (ujasiri),na roho ya upendo (tunda la Roho),pamoja na moyo wa kiasi (self discipline) – 2 Timotheo 1:7. Hii ina maana woga,hofu na mashaka hayatokani na Mungu,bali yanatokana na shetani.

Na kama tunakubaliana kwamba roho ya nguvu imetokana na Mungu,basi ina maana Mungu ameweka uwezo /ujasiri ndani yako ili uweze / ufanikiwe/ ufanye yale yanayoonekana magumu. Ukumbuke ya kwamba roho ya utumwa,ndiyo iletayo “hofu” . Kuokoka” ni kuzaliwa mara ya pili,mahali ambapo ile roho ya nguvu inahuishwa ndani yako,na ndipo unapopokea roho ya uwana ( Warumi 8:14).

Hii ina maana roho ya nguvu aliyokupa Mungu,ilififiishwa na utumwa wa dhambi,hata mlango wa hofu ukawa wazi na hatimaye roho ya nguvu ikapoteza nafasi yake. Lakinikwa tendo moja la kuja kwa Kristo,roho ya nguvu/ujasiri inarejeshwa na hali ya uwana.

Lakini Je mbona wasiokoka wengine ni majasiri kuliko waliookoka? – Ni kweli,wapo watu wa dunia hii ambao ni majasiri kuliko wana wa nuru,hii ni kwa sababu adui amekuwa akiwajaza ujasiri katika kutenda maovu,kwa maana anajua hao ni mali yake. Lakini ujasiri wa mema ni kazi ya Bwana ambayo ameachilia ndani yako tayari.

Tujifunze kwa Petro na Yohana tu kwa kifupi,akina Petro na Yohana ambao kwanza walikuwa ni watu wasio na elimu,lakini si hivyo tu,walikuwa ni watu wasiokuwa na ushawishi mkubwa katika jamii,hawakuwa matajiri lakini walikuwa na ujasiri mkubwa,ujasiri wao ulitokea wapi?

Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.  Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu.’‘ Matendo 4:13-14

Mambo muhimu ya kujifunza kuhusu ujasiri (Katika Matendo 4:13-14);

  1. Ujasiri ni jambo la ndani,lenye matokeo ya nje “walipouona ujasiri”. Hii ina maana ujasiri kuna mahali umetokea na hatimaye ukaweza kuonekana nje,watu wakauona ujasiri.
  2. Ujasiri hautegemei elimu yako / maana Petro na Yohana hawakusoma.
  3. Ujasiri unastajabisha watu,wasioamini na wanaoamini wanapigwa na butwaa wanapouona ujasiri.
  4. Ujasiri unamtambulisha Mungu uliyenaye. Maana walipowaona Petro na Yohana wakawatambua walikuwa na Yesu. Kumbe mtu wa Mungu mwenye ujasiri hawezi kumficha Yesu kwa maana hata kama hatasema chochote,bali watu watatambua na kumwona Yesu.
  5. Ujasiri huwafunga vinywa wasioamini! Mstari wa 14
  6. n.k

Kwa nini watu hukosa ujasiri?

Ukweli nikwamba ujasiri ni jambo la rohoni sana,na ni la kiungu,hivyo moja ya kitu kikubwa ambacho adui anakiwinda na kukipiga ni eneo la ujasiri. Kwa maana mtu awaye yote asipokuwa na ujasiri basi atakuwa na hofu,

na hapo kwenye hofu ndipo kwenye mlango wa adui ibilisi. Kitendo cha kuogopa na kusema “mimi siwezi ” kitendo hicho tu,kinatosha kushindwa kabla ya kushindwa kwenyewe!

Hivyo wengi wamejikuta wamepoteza ujasiri kwa sababu kwanza wamemwacha au kumkataa Yesu,na wale waliompokea Yesu wamekuwa wakijitamkia kushindwa kisha hofu nayo huchukua nafasi na gafla hata wakijaribu wanashindwa kweli!. Lakini pili,ujasiri unakosekana pale ambapo pana “uovu / dhambi” .

Dhambi ni adui namba moja wa kuondoa ujasiri!!! Maana dhambi ni adui wa haki! popote pale palipo na dhambi,basi ujue ujasiri wa haki upotea,kwa maana huwezi kusimama kijasiri kwenye haki ikiwa wewe mwenyewe ni mpenda kutenda dhambi!

Je ujasiri,unahuitaji?

Bila shaka ndio,kwa maana hakuna mtu ambaye anaipenda hofu. Kwa kuwa ujasiri ni jambo la kiroho,basi inawezekana hata leo kuvikwa roho hii ya ujasiri katika maeneo yako,labda katika eneo la utumishi,au eneo la kazi n.k.

Kitu pekee kitakachokufanya uwe jasiri ni Roho mtakatifu,kwa njia ya maombezi. hata hivyo lazima uanze kuthubutu kufanya yale uliyokuwa ukiona huyawezi,kwa msaada wa Roho mtakatifu katika maombezi,inawezekana. Ninaomba tuombe pamoja sasa

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.

Kwa maombi, maombezi na ushauri (+255) 0781 001 002

Mch. Gasper Madumla

Whatsapp namba +255 746 446 446

UBARIKIWE.

4 thoughts on “UJASIRI

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.